Vifurushi Bora. Ushauri wa bure. Gharama nafuu.
Tuna vifurushi bora kwa biashara mpya, biashara kubwa, na hata kampuni! Chagua kimoja, nasi tutafanya kazi yetu kikamilifu. Vifurushi vyote vinajumuisha VAT (18%).
Mtoto
Kizuri kwa waanzilishi wa biashara.
Tsh 248,000
- Nembo (logo) ya biashara
- Maudhui 5 ya Instagram
- Kibao cha lipa namba cha glasi (A6)
- Bango la logo la glasi “la ukutani” (30cm)
- Bango kubwa la mita 1 la huduma zako
- Usajili wa jina la biashara + lipa namba
- Tisheti 2 zilizochapishwa logo yako
Mama
Kizuri kwa biashara kubwa.
Tsh 655,000
Kifurushi cha MTOTO na,
- Pisi 100 ya stika za delivery
- Mifuko pisi 100 yenye logo yako
- Machapisho 10 ya Instagram
- Muhuri mkubwa wa vifungashio
- Vitabu 5 vya ankara (A5)
- Tisheti 3 zilizochapishwa logo yako
Baba
Kizuri kwa kampuni na mashirika.
Tsh 1,520,000
Kifurushi cha MAMA na,
- Pisi 5 za kalenda (A4-A3)
- Pisi 5 za wasifu wa kampuni (A5/A4)
- Vipeperushi 100 (A5) + Vitambulisho 10
- Bango moja kubwa “roll-up” (2m)
- Vitabu 10 vya risiti za kampuni (A5)
- Tisheti 5 zilizochapishwa logo yako
Maswali ya mara kwa mara kuhusu vifurushi vyetu.
Hapa kuna majibu ya haraka kwa baadhi ya maswali kuhusu vifurushi vyetu. Wasiliana nasi wakati wowote ikiwa unahitaji usaidizi zaidi, tuko hapa kukuhudumia.
Nani anaweza kununua vifurushi hivi?
Mtu yeyote! Tuna vifurushi tofauti kuendana na aina zote za wateja; Iwe ni mteja anaye anzisha biashara, mmiliki wa biashara kubwa, mmiliki wa kampuni, na hata mashirika! Unaweza kuchagua kifurushi kinachoendana nawe wakati wowote.
Mnapokea njia gani za malipo?
Tunapokea njia nyingi za malipo ili wateja wetu wajisikie huru kuchagua: M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money | Equity Bank, CRDB (USD, TZS) | Crypto (USDT, USDC) | Selcom Pay | AzamPesa
Naweza kufika ofisini kabla sijalipia?
Ndiyo, kabisa! Unaweza kutembelea ofisi yetu iliyopo Sinza E – Dar Es Salaam, Tanzania ili tuweze kujadiliana ana kwa ana kabla ya kulipia kifurushi chako. Hakika huu utakuwa uamuzi bora kwako kwani tutakuwa na wakati wa kushauriana na kupendekeza kifurushi au huduma bora kwa biashara/kampuni yako.
Hatua gani itafuata baada ya malipo?
Kwanza, tutaandika oda yako kwenye data zetu za wateja na kukupa risiti ya malipo kwa ajili ya ulinzi. Kisha tutaanza kufanyia kazi oda yako papo hapo au siku inayofuata ikiwa kuna wingi wa kazi. Tutafanya kazi nawe kwa karibu na kutuma ripoti ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinaendelea vizuri bila matatizo yoyote.
Naweza kurudishiwa pesa yangu?
Ndiyo! Unaweza kurejeshewa pesa yako ikiwa tulifanya makosa kwa upande wetu. Hakikisha unahifadhi stakabadhi yako ya malipo kwaajili ya dharura yoyote, vinginevyo hatutaweza kukusaidia kurejesha pesa yako.