HARUSI KIDIGITALI
Miundo mizuri ya kadi. Usaidizi. Bei poa!
Epuka gharama zisizo za lazima na uokoe muda pia wa kusambaza kadi za HARUSI, SEND-OFF au MICHANGO nyumba hadi nyumba! Tumia kadi za kidigitali kutoka Hamia Digital popote ulipo.
Mfano wa kadi zetu za kurasa moja.
Mfano wa kadi zetu za kurasa mbili.
Tsh 1000
Kadi ya kurasa moja, mfano 👇

- Design ya kadi (kurasa moja)
- Tunatuma kadi kwa WhatsApp
- SMS kwa jina: HARUSI au SEND-OFF
- Tunapiga simu kukumbusha waalikwa
QR-Code kwa ajili ya ku-scanTutafika ukumbini kwako ku-scan kadiZawadi za bure kwa maharusi 😍Tovuti ya maharusi(ONA MFANO)
Tsh 1500
Kurasa mbili + Timu ya kuscan

- Design ya kadi (kurasa mbili)
- Tunatuma kadi kwa WhatsApp
- SMS kwa jina: HARUSI au SEND-OFF
- Tunapiga simu kukumbusha waalikwa
- QR-Code kwa ajili ya ku-scan
- Tutafika ukumbini kwako ku-scan kadi
Zawadi za bure kwa maharusi 😍Tovuti ya maharusi(ONA MFANO)
Tsh 2000
Kurasa mbili + Timu + Tovuti bure

- Design ya kadi (kurasa mbili)
- Tunatuma kadi kwa WhatsApp
- SMS kwa jina: HARUSI au SEND-OFF
- Tunapiga simu kukumbusha waalikwa
- QR-Code kwa ajili ya ku-scan
- Tutafika ukumbini kwako ku-scan kadi
- Zawadi za bure kwa maharusi 😍
- Tovuti ya maharusi (ONA MFANO)
Maswali muhimu.
Baadhi ya maswali muhimu yanayoulizwa mara kwa mara na wateja wetu kuhusu huduma hii.
Nani atafanya design ya kadi na kusambaza?
Tunayo miundo tofauti ya kadi za kurasa moja na kurasa mbili, hivyo tutakutumia list ya kadi zote kisha uchague uipendayo. Kisha tutajaza maelezo ya shughuli yako kwenye kadi uliyochagua na tutakutumia sample uone kama ni sawa, baada ya hapo tutaunda kadi za waalikwa wako wote sawa sawa na sample hiyo na kuanza kuzisambaza mara moja! Kazi yako itakuwa moja tu ambayo ni kutupatia maelezo ya shughuli yako pamoja na majina na namba za simu za waalikwa.
Mtanisaida kuhakiki kadi ukumbini?
Ndio! Tutakusaidia kuhakiki kadi za waalikwa wote ukumbini kwenye shughuli yako. Unatakiwa kununua kadi za Tsh 1500 au Tsh 2000 ili vijana wetu wafike ukumbini na kukusaidia kwenye uhakiki wa kadi zote kwa uzoefu mkubwa na ubora wa hali ya juu.
Naweza kupata idadi ya kadi chache za kuchapisha?
Bila shaka! Baadhi ya wateja wetu wamekuwa wakiomba idadi chache ya kadi mfano 10/20 zichapishwe kwa ajili ya wakwe au wageni maalum, hivyo ondoa shaka kwasababu tutachapisha kadi zako pia ukihitaji.
Nafanyaje malipo ya huduma hii?
Kabla ya kuanza kazi yako, utatakiwa kulipia 50% ya jumla ya malipo. Tunapokea malipo kwa mitandao ya simu na sarafu za kidigitali kama vile: BTC | ETH | USDT | USDC
Kazi itakamilika kwa muda gani?
Baada ya kupokea 50% ya malipo kutoka kwako, tutaanza kufanya kazi yako mara moja! Ndani ya saa 24 tutakuwa tumemaliza kuunda kadi zote, kutuma kwa WhatsApp na kutuma kwa SMS za kawaida. Baada ya hapo tutakuwa tukishirikiana na kamati au maharusi ili kutuma kadi zitakazo ongezeka, kutuma SMS za kukumbushia siku ya shughuli, pamoja na kuwapigia simu waalikwa. Malipo yaliyobaki (50%) utayamalizia siku moja kabla ya shuguli yako baada ya kuhakikisha zoezi zima la usambazaji wa kadi na ukumbushaji wa shughuli umekamilika.
Mnatoa huduma nyingine zozote za harusi?
Ndio! Tunatoa huduma nyingine zinazohusiana na harusi, send-off, mikutano na kadhalika, huduma hizo ni kama vile;
- Photoshoot – Tsh 250,000
- Video Production – Tsh 1,300,000
- Bango la harusi + stendi (mita 3×4) – Tsh 170,000
Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi: +255749987122