Pata huduma bora za ubunifu wa picha na uchapishaji
Tuna utaalamu wa kutoa miundo ya kipekee na uchapishaji wa viwango vya juu kabisa, wasiliana nasi tufanye wazo lako kuwa hai. Huduma zetu zinakufikia popote ulipo ndani na nje ya Tanzania, karibu!
Chagua Huduma
Ubunifu
Tunabuni karibu kila kitu! Tovuti, Nembo za biashara au kampuni, Vipeperushi, Mabango, Maudhui ya mitandao ya kijamii na zaidi.
Uchapishaji
Mifuko ya kubebea bidhaa, Tisheti, Kofia, Vikombe, Kalenda, Risiti, Picha mbao au kioo, Mabango na nyenzo zingine za utangazaji.
Usimamizi
Tunakusaidia kusimamia mitandao yako ya kijamii au tovuti ya biashara/kampuni yako na kushirikiana na wateja wako kwa ufasaa kabisa.
KUHUSU SISI
Sehemu ya kuaminika ya ubunifu na uchapishaji
Hamia Digital ni kati ya timu moja wapo inayoaminika zaidi kwenye tasnia ya ubunifu na uchapishaji. Tunao uzoefu mzuri na timu yenye ujuzi mkubwa kuhakikisha kazi zetu zinakidhi viwango vya juu kabisa ili kuweka tabasamu kwenye nyuso za wateja wetu wakati wote, hutojutia kufanya kazi nasi.
- Kazi za viwango vya juu
- Miaka 7+ ya uzoefu
- Timu yenye ujuzi mkubwa
- Tunakamilisha kazi kwa wakati
Huduma Zetu
Timu yetu ipo tayari kukuhudumia! Iwe ni miundo ya kibunifu au huduma za uchapishaji, tupo tayari kupokea kazi yako na kutoa matokeo bora kwa wakati.
Kutengeneza Tovuti
Biashara bila tovuti ni sawa na gari lisilo na mafuta, wasiliana nasi leo tukutengenezee tovuti nzuri itakayoendana na biashara yako.
Kadi za Kidigitali
Okoa gharama na muda wa kusambaza kadi za harusi, send-off, nk! Tunakusaidia kusambaza kadi kwa wageni wako wote kidigitali.
Nembo za Biashara
Biashara nzuri huanza na nembo nzuri! Tunakutengenezea nembo itakayotambulisha bisahara au kampuni yako popote pale.
Vifaa vya Matangazo
Tunabuni na kuchapisha vifaa vya utangazaji ikiwa ni pamoja na Vipeperushi, Mabango, Stika, na zaidi! Weka oda yako leo.
Huduma za Usimamizi
Tunakusaidia kusimamia na kuendesha mitandao yako ya kijamii au tovuti ya biashara/ kampuni na kukutumia ripoti kila wiki.
Vifaa vya Kazi
Tunauza na kuchapisha vifaa vya maofisi kama vile mifuko, tisheti, kofia, vitambulisho, risiti, kalamu, vikombe, vitabu, kalenda, beji, nk.
Baadhi ya Kazi Zetu
Baadhi ya Maoni ya Wateja Kuhusu Hamia Digital

Timu ya Hamia Digital ni bora sana! Muundo ambao nimeagiza unaojumuisha nembo ya kampuni yetu na mabango umekuwa wa kipekee sana. Timu yangu na mimi tumeridhika sana. Shukrani kwao!

Zurich Upholstery
Founder

Kusema kweli, nimepata mahali pazuri pa kupata miundo yote ninayotaka kwa ajili ya biashara yangu. Hamia Digital daima hutoa miundo bora inayoendana na biashara yangu, ninashukuru na nimefurahi kufanya nao kazi.

Neyscassava
Founder

Nilijaribu huduma zao mara moja, na kuishia kufanya kazi nao wakati wote! Wameunda tovuti bora kwa biashara yangu, nembo ya kampuni, lebo za mavazi na maudhui ya mitandao ya kijamii ya kuvutia kabisa.

Eline Designs
Founder
Maswali Yanayoulizwa Sana na Wateja
Baadhi ya majibu ya maswali yanayoulizwa zaidi na wateja wapya. Ikiwa hujapata jibu la swali lako usisite kuwasiliana nasi wakakati wowote, tupo hewani kukuhudumia!
Nyie ni kina nani?
Sisi ni Hamia Digital, iliyoanzishwa tangu 2017. Sisi ni wataalam katika huduma za kibunifu na uchapishaji! Fanya kazi nasi na hutojutia kabisa, tunahitaji uaminifu kidogo tu kutoka kwako kisha uone matokeo ya kazi zetu. Moja ya jukumu letu ni kuifanya biashara au kampunia yako ivutie zaidi na kukuletea wateja wapya kwa miundo yetu ya kipekee, huduma za uchapishaji, huduma za usimamizi na kampeni za uuzaji (masoko). Kwa sasa tunapatikana Dar Es Salaam – Tanzania, Mtaa wa Sinza E.
Mnatoa huduma gani?
Tunatoa karibu kila huduma katika sekta ya ubunifu na uchapishaji, pia tunafanya kazi na washirika wengine wengi katika sekta hii, kwa hivyo tunakuhakikishia kwamba tutakabidhi kazi yako kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati kabisa bila kujali ukubwa wake!
Iwe unahitaji tovuti ya biashara au kampuni yako, kadi za kidijitali, nembo za biashara au kampuni, vipeperushi, mabango, na nyenzo nyinginezo za utangazaji, usimamizi wa mitandao ya kijamii pamoja na huduma zote za uchapishaji iwe ni tisheti yenye nembo yako, vikombe, kofia, mifuko ya kufungashia bidhaa, kalamu, picha na mengine mengi.
Pia tunatoa huduma za usimamizi wa kampeni za uuzaji (masoko), iwe ni kampeni za uuzaji mtandaoni au matukio ya moja kwa moja, tuko tayari kukuhudumia!
Ninaweza kupata huduma zenu mtandaoni?
Hakika! Huduma zetu nyingi zinapatikana mtandaoni. Unaweza kupata huduma zetu kwa ubora kabisa mtandaoni bila kujali eneo ulipo hata ikiwa ni nje ya Tanzania.
Na pia usijali hata ikiwa unaagiza bidhaa za kuchapishwa, bado tunaweza kuchapisha bidhaa zako na kukutumia ulipo kupitia basi za mikoani na kampuni za usafirashaji. Utapokea bidhaa zako ndani ya saa 24 hadi siku 3 kutokana na mkoa/nchi uliyopo.
Itachukua muda gani kupokea oda yangu?
Inategemea! Makadirio ya muda hutokana na huduma uliyochagua au eneo utakaloletewa, mara nyingi baadhi ya wateja wetu hupokea kazi zao au bidhaa ndani ya saa 24 na wengine hupokea siku chache baada ya kuagiza.
Kadi za kidigitali ndio nini?
Kadi za kidigitali ni zile ambazo huwezi kushika mkononi, zinapatikana mtandaoni pekee. Kadi hizi husaidia kupunguza gharama za usambazaji kwa wageni wako (hakuna tena uwasilishaji wa nyumba kwa nyumba) hivyo huokoa muda na gharama za usambazaji.
Ni wewe tu kuweka oda! Tutaunda kadi zako, tutazituma kwa wageni wako kupitia WhatsApp, tutatuma SMS za kawaida pia, SMS hizo zitakuwa na kichwa cha tukio lako (kwa mfano: HARUSI | SEND-OFF | MCHANGO | GRADUATION | KIKAO), na hatimaye kuwapigia simu wageni wako wote ili kuhakikisha kuwa kila mtu amepokea kadi zao za mwaliko kidigitali pasipo shida yeyote.
Tutafanya kazi nawe kwa ukaribu kabisa na kukutumia ripoti hadi tukio lako likamilike ili kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa!
Mnatoa huduma ya usafirishaji wa bidhaa?
Ndiyo! Tunafanya huduma za usafirishaji kwa wateja wetu ndani ya Dar Es Salaam na hata mikoa mingine. Tunashirikiana na kampuni za usafirishaji zinazoaminika ili kuhakikisha kuwa bidhaa zako zinakufikia kwa usalama na kwa wakati mahali ulipo.
I need service in English.
Don’t worry, look at the bottom left of our website and you will see a pop-up language translation button then select English. You can also chat with us in English directly on WhatsApp. You’re welcome!
Tunatuma Bidhaa
Kwa sasa tunasafirisha bidhaa za wateja wetu kwa maeneo yaliyoorodheshwa hapo chini tu, tunatumai kutanua huduma hii siku zijazo.
Maeneo tunayotuma bidhaa:
Tunafanya kazi na wasafirishaji wanaoaminika kimataifa ili kuhakikisha kuwa bidhaa yako inafika kwa usalama na kwa wakati, pia tunapokea njia mbalimbali za malipo.
- Tanzania nzima
- Zanzibar, Kenya
- Rwanda, Burundi
- Uganda, Congo
- Africa Kusini
- Lipa kwa Simu
- CRDB, Equity Bank
- Crypto: USDT, USDC
- SelcomPay, AzamPesa
- TZS, KSH, USD, EURO
